

Lugha Nyingine
Sherehe za Mwaka Mpya wa Jadi wa China zavutia watu nchini Zimbabwe
Wanafunzi wa Zimbabwe wakijifunza sanaa ya Wushu ya China kutoka kwa msanii wa kikundi kinachotembelea Zimbabwe kutoka Kituo cha Mafunzo ya Wushu cha Shaolin cha Mkoa wa Henan, nchini China wakati wa shughuli ya mabadililshano ya utamaduni mjini Harare, Zimbabwe, Januari 31, 2024. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua)
HARARE - Shughuli ya mabadilishano ya kitamaduni imefanyika Harare, Zimbabwe, Jumatano kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ambapo shughuli hiyo katika Shule ya Sekondari ya Urafiki kati ya China na Zimbabwe huko Hatcliffe, Harare ilishirikiwa na Balozi wa China nchini humo Zhou Ding, na Waziri wa Elimu ya Msingi na Sekondari wa Zimbabwe Torerai Moyo, miongoni mwa wengine.
Ngoma za kuvutia za kienyeji na za wanafunzi kutoka shuleni ziliwatumbuiza wageni wa China huku Wazimbabwe wakishangazwa na maonyesho ya sanaa ya wushu ya China mazingaombwe na ngoma za Kichina yaliyofanywa na kikundi kinachotembelea Zimbabwe kutoka Kituo cha Mafunzo ya Wushu cha Shaolin cha Mkoa wa Henan, nchini China.
"Maonyesho haya yatafungua dirisha kwa ajili yenu kwa mambo ya ajabu ya sanaa na utamaduni wa China. Natumai nyote mtafurahia na ninawatakia nyote kutimiza ndoto zenu katika siku zijazo, na kuchangia katika maendeleo ya kisasa na ya kiviwanda ya Zimbabwe," amesema Zhou.
Zhou amesisitiza tena uungaji mkono wa China kwa maendeleo ya Zimbabwe, hasa katika sekta ya elimu.
Kwa upande wake, Moyo amesema sherehe hiyo inasaidia kuimarisha uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili na kusisitiza umuhimu wa uanuai na ujumuishaji wa taasisi za elimu za Zimbabwe.
"Kwa kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa pamoja, siyo tu kwamba tunaheshimu jamii ya Wachina, lakini pia tunaongeza hali ya mshikamano kati yetu sote. Elimu ni chombo chenye nguvu kinachovunja mipaka na kupanua upeo. Inatuwezesha kukumbatia tamaduni, mila na mitazamo tofauti, kuhimiza mawazo ya kimataifa ambayo ni muhimu katika Dunia ya sasa iliyounganishwa," amesema.
Katika shughuli hiyo, wanafunzi wenyeji walioshiriki kwenye shughuli hiyo walifurahia fursa ya kujifunza sanaa ya wushu ya China kutoka kwa kikundi kinachotembelea Zimbabwe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma