

Lugha Nyingine
Uwekezaji wa miundombinu wa China wachochea ukuaji wa uchumi barani Afrika
NAIROBI - Uwekezaji mkubwa wa miundombinu wa China barani Afrika unachochea ukuaji wa uchumi wa bara hilo, Katibu Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Vincent Nmehielle amesema Alhamisi.
Nmehielle amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi, Kenya, kwamba nchi ya hiyo ya Asia imetoa mitaji kwa miradi ya miundombinu kupitia makubaliano ya pande mbilimbili na nchi za Afrika na pia kupitia taasisi za kifedha za pande nyingi za maendeleo.
"Kwa ujumla, natarajia miradi ya miundombinu iweze kufungua uchumi kwa namna ya kuwezesha nchi zioneshe umuhimu wake, ikiwa ni barabara au daraja inaweza kuufanya usafirishaji wa bidhaa uwe rahisi zaidi, na hiki ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi," amesema kwenye mkutano na wanahabari kuhusu maendeleo yaliyofikiwa katika maandalizi ya Mkutano wa 59 wa Mwaka wa AfDB ambao umepangwa kufanyika Nairobi, Mei 27-31.
Mkutano huo unatarajiwa kukaribisha wajumbe 4,000 wakiwemo pamoja na mawaziri wa fedha kutoka nchi za Afrika, maofisa waandamizi wa AfDB, washirika wa maendeleo pamoja na sekta ya kibinafsi.
Nmehielle ameongeza kuwa mitaji kutoka China imeendana na kuungana mkono na mitaji kutoka kwa wafadhili wengine wa kigeni pamoja na rasilimali za ndani ya Afrika katika kupunguza pengo la maendeleo ya miundombinu barani Afrika ambalo linakadiriwa kufikia dola za kimarekani bilioni 170 kila mwaka.
China na AfDB kwa pamoja zilianzisha Mfuko wa Afrika Kukua kwa Pamoja ili kufadhili miradi ya maendeleo barani Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma