

Lugha Nyingine
Afrika CDC yapongezwa kwa kulinda afya ya umma barani Afrika
Picha hii iliyopigwa tarehe 31, Januari ikionesha makao mkuu ya Afrika CDC mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimeadhimisha miaka saba tangu kuanzishwa kwake, na kupongezwa kwa mchango wake katika kuboresha huduma za afya ya umma barani Afrika.
Hafla maalum ya maadhimisho ya kutimiza miaka saba tangu kuanzishwa kwa kituo hicho, imefanyika mjini Addis Ababa, chini ya kaulimbiu ya “Safari ya vitendo na kujitolea kulinda usalama wa afya barani Afrika,” ikiangazia mafanikio ya kituo hicho katika kusaidia mipango ya afya ya umma, kuimarisha uwezo wa taasisi za afya za umma, kuzuia, kudhibiti na kuitikia kwa haraka na kwa ufanisi matishio ya magonjwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo hicho Bw. Jean Kaseya amesema tangu kituo hicho kianzishwe Januari 2016, kimehimili matishio mbalimbali ya afya ya umma, kuanzia mlipuko wa virusi vya Ebola na hadi janga la hivi karibuni la COVID-19.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma