

Lugha Nyingine
Serikali ya Tanzania yasema tathmini ya nchi nzima kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi inaendelea
Serikali ya Tanzania imesema timu ya wataalamu wa Ofisi ya Rais (Muungano na Mazingira) kwa kushirikiana na Idara za kisekta imeanza tathmini ya athari za mabadiliko ya tabianchi nchi nzima.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Selemani Jafo ameliambia Bunge la Tanzania siku ya Jumatano kuhusu kuendelea kufanyika kwa tathmini hiyo ya kimazingira wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtambwe kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Khalifa Mohamed Issa.
Mbunge huyo alisema visiwa vya Unguja na Pemba vimeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na kusababisha baadhi ya makazi ya watu kuzama majini.
Katika swali lake mbunge huyo alisema kuwa visiwa hivyo vimeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na kusababisha baadhi ya maeneo kuzama. Alitaka kujua ni lini serikali itafanya utafiti na kuja na hatua gani za muda mfupi na mrefu za kukabiliana na hali hiyo.
Akijibu Dk Jafo amesema serikali imeanza ujenzi wa ukuta katika eneo hilo na kuongeza kuwa timu ya wataalamu kwa kushirikiana na idara za kisekta imetumwa kufanya tathmini nchi nzima.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma