16 wauawa, 25 wajeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Marekani Magharibi mwa Iraq

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 04, 2024

Picha hii iliyopigwa Februari 3, 2024 ikionyesha gari lililoharibiwa baada ya mashambulizi ya anga ya Marekani huko Anbar, Iraq. (Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Februari 3, 2024 ikionyesha gari lililoharibiwa baada ya mashambulizi ya anga ya Marekani huko Anbar, Iraq. (Xinhua)

BAGHDAD - Msemaji wa serikali ya Iraq Basim al-Awadi amesema Jumamosi kwamba mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Kundi la Hashd Shaabi magharibi mwa Iraq yameua watu 16, wakiwemo raia, na kujeruhi wengine 25, huku akiyaelezea mashambulizi hayo ya anga kuwa ni "uvamizi wa wazi."

Al-Awadi ameliambia Shirika la Habari la Iraq (INA) kwamba "serikali ya Marekani umekiuka mamlaka ya Iraq wakati ndege hiyo ilipofanya mashambulizi ya anga kwenye kambi za vikosi vyetu vya usalama katika maeneo ya Akashat na al-Qaim, pamoja na maeneo jirani ya kiraia.

Al-Awadi pia amekanusha ripoti zilizodai kuwa kulikuwa na uratibu kati ya serikali ya Iraq na ile ya Marekani kuhusu mashambulizi hayo ya anga, akisisitiza kwamba ripoti hizi ni "madai ya uongo yenye lengo la kupotosha maoni ya umma ya kimataifa na kukwepa kuwajibika kisheria kwa uhalifu huu," kwa mujibu wa INA.

Vile vile amesema, serikali ya Iraq inaamini kuwa kuwepo kwa vikosi vya muungano wa kimataifa nchini Iraq kumekuwa tishio kwa usalama na uthabiti wa Iraq na kunasababisha Iraq kuingia kwenye migogoro ya kikanda na kimataifa.

Al-Awadi ameonya kwamba mashambulizi ya hivi karibuni ya anga yameiweka Iraq na kanda nzima kwenye hatari, na kuongeza, "Iraq inasisitiza kukataa kufanya ardhi yake kuwa uwanja wa mapambano."

Kamandi Kuu ya Marekani ilisema katika taarifa yake siku ya Ijumaa kwamba vikosi vya Marekani vilifanya mashambulizi ya anga katika maeneo zaidi ya 85 nchini Iraq na Syria dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) na makundi ya wanamgambo.

Mashambulizi hayo ya anga ya Marekani yamekuja kujibu mashambulizi ya hivi majuzi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran ambayo yalisababisha Wamarekani kuuawa kwa mara ya kwanza tangu mgogoro kati ya Israel na Hamas kuzuka Oktoba 7, 2023.

Picha hii iliyopigwa Februari 3, 2024 ikionyesha nyumba iliyobomolewa baada ya mashambulizi ya anga ya Marekani huko Anbar, Iraq. (Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Februari 3, 2024 ikionyesha nyumba iliyobomolewa baada ya mashambulizi ya anga ya Marekani huko Anbar, Iraq. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha