

Lugha Nyingine
Kampuni za China zatoa msaada wa vifaa vya kudhibiti kipindupindu kwa Zimbabwe
Viongozi wakipokea vifaa vya kudhibiti kipindupindu vilivyotolewa na Shirikisho la Wafanyabishara wa China nchini Zimbabwe (CCEZ) mjini Harare, Zimbabwe, Februari 2, 2024. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua)
HARARE - Kampuni za China nchini Zimbabwe chini ya Shirikisho la Wafanyabiashara wa China nchini Zimbabwe (CCEZ) siku ya Ijumaa zilitoa msaada wa vifaa vya kudhibiti kipindupindu vyenye thamani ya dola za Marekani 10,000 kwa nchi hiyo ya Afrika ambavyo ni pamoja na dawa za kuua vijidudu, mavazi ya kujikinga, mahema na vyakula kwa Hospitali ya Magonjwa ya Kuambukiza ya Beatrice Road mjini Harare.
"Ni muhimu kwa jumuiya za wafanyabiashara kushirikiana ili kutoa msaada," amesema Liu Baixue, Naibu Mwenyekiti wa CCEZ, baada ya hafla ya kukabidhi msaada.
“Msaada huo siyo tu unaonyesha uwajibikaji wa kijamii wa kampuni hizo za China lakini pia unaashiria mshikamano na uhusiano kati ya watu wa China na Zimbabwe,” Liu ameongeza.
CCEZ ina wanachama zaidi ya 80, ikiwa ni pamoja na mashirika yanayomilikiwa na serikali ya China na kampuni za zilizoorodheshwa katika masoko ya mitaji na hisa ya China katika sekta mbalimbali kama vile madini, viwanda, uzalishaji wa umeme na vifaa.
Gideon Mapokotera, Ofisa Rasilimali Watu katika Wizara ya Afya na Malezi ya Watoto ya Zimbabwe, amezishukuru kampuni hizo za China kwa msaada wao, akiuona kama kinga kwenye mkono katika mapambano dhidi ya kipindupindu.
"Wachina daima wamekuwa marafiki wazuri wa Zimbabwe. Wameleta vitu mbalimbali ... na hizi zitasaidia sana kuwapa motisha wafanyakazi wetu, na kufikia jamii yetu," amesema.
Hadi sasa, visa vya maambukizi ya Kipindupindu vimerekodiwa katika wilaya nyingi kati ya 64 za Zimbabwe. Siku ya Jumatatu, mpango wa chanjo dhidi ya kipindupindu unaolenga watu milioni 2.3 ulizinduliwa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma