Rais wa Namibia Geingob afariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitalini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 05, 2024

Picha ya kumbukumbu iliyopigwa Machi 14, 2022 ikimwonyesha Hage G. Geingob wakati akizungumza mjini Windhoek, Namibia. (Xinhua/Chen Cheng)

Picha ya kumbukumbu iliyopigwa Machi 14, 2022 ikimwonyesha Hage G. Geingob wakati akizungumza mjini Windhoek, Namibia. (Xinhua/Chen Cheng)

WINDHOEK - Rais wa Namibia Hage G. Geingob ameaga dunia mapema Jumapili wakati alipokuwa akipokea matibabu ya saratani kwenye hospitali katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Windhoek, ofisi ya rais imetangaza. Amefariki akiwa na umri wa miaka 82.

"Nikiwa kwa huzuni na masikitiko makubwa ninawajulisha kuwa mpendwa wetu Dkt. Hage G. Geingob, Rais wa Jamhuri ya Namibia, amefariki dunia leo Jumapili tarehe 4 Februari 2024 majira ya saa 06:04 usiku (Kwa saa za Namibia) katika Hospitali ya Lady Pohamba alikokuwa akipokea matibabu kutoka kwa timu yake ya matibabu," Kaimu Rais Nangolo Mbumba amesema katika taarifa kwenye ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa Ikulu ya Namibia.

Geingob amekuwa akihudumu nafasi ya rais wa tatu wa Namibia tangu Machi 21, 2015, na alichaguliwa tena kuwa rais kwa awamu nyingine ya miaka mitano mwaka 2019. Aliwahi kuhudumu nafasi ya waziri mkuu wa nchi hiyo Mwaka 1990-2002 na 2012-2015, pamoja na majukumu mengine muhimu ya kiwaziri na uongozi.

"Timu yake ya matibabu... imekuwa ikijaribu kila iwezalo kuhakikisha kuwa Rais wetu anapona," imesema taarifa hiyo."Kwa masikikito, licha ya juhudi za dhati za timu hiyo kuokoa maisha yake, kwa huzuni, wananchi wenzangu wa Namibia, Rais Geingob amefariki dunia."

"Taifa la Namibia limepoteza mtumishi mashuhuri wa watu, alama ya mapambano ya ukombozi, msanifu mkuu wa katiba yetu na nguzo ya nyumba ya Namibia," imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imetoa wito kwa Wanamibia "kubaki watulivu na wamoja wakati ambapo serikali inashughulikia mipango yote muhimu ya kitaifa, maandalizi na itifaki nyingine."

Siku ya Jumamosi, Makamu Rais Mbumba aliwaambia watu wa nchi nzima kwamba Geingob alikuwa katika hali mbaya lakini ni ya tulivu baada ya kupata matibabu ya saratani katika Hospitali ya Lady Pohamba huko Windhoek, mji mkuu wa nchi hiyo.

Januari 19, Ikulu ya Namibia ilisema timu ya matibabu ya Geingob iligundua seli za saratani kufuatia uchunguzi wa biopsy. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha