Hafla ya kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China yafanyika nchini Zambia

(CRI Online) Februari 05, 2024

Hafla ya kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China iliyoandaliwa na Ubalozi wa China nchini Zambia, imefanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lusaka, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zambia, Chipoka Mulenga.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zambia, Waziri Mulenga amesema Rais Hakainde Hichilema amewatakia Wachina heri na mafanikio katika mwaka mpya, na kusema mwaka wa Dragoni unaashiria ukuaji, ustawi na mambo mema.

Naye Balozi wa China nchini Zambia, Du Xiaohui amesema, katika miaka 60 iliyopita, biashara na mabadilishano kati ya watu wa nchi hizo mbili vimetoa mchango mkubwa katika urafiki kati ya nchi hizo mbili, na kutumia vizuri fursa zinazotokana na ushirikiano kati ya nchi hizo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha