Lugha Nyingine
Umoja wa Mataifa waahidi kutoa mafunzo ya kiufundi kwa vikosi vya usalama vya Somalia
Tume ya Usaidizi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOS) imeahidi kutoa mafunzo ya kiufundi kwa vikosi vya usalama vya nchini humo wakati wa kipindi cha mpito.
Tume hiyo inayotoa msaada wa ugavi kwa Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumamosi mjini Mogadishu, kuwa mafunzo hayo yatahakikisha operesheni endelevu na utunzaji wa vifaa vya vikosi vya usalama.
Ofisa msimamizi wa UNSOS Qurat-Ul-Ain Sadozai amesisitiza makabidhiano salama ya kambi saba za kijeshi wiki iliyopita, na kupongeza uhusiano kati ya ATMIS, serikali ya Somalia na Tume yake, huku akiahidi kuendeleza uratibu na uungaji mkono wa zoezi hilo.
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
Mandhari ya kushangaza ya “Barabara Kuu inayoning’inia kwenye Miteremko ya Vilima” wakati wa theluji
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma