

Lugha Nyingine
Rais mpya wa Namibia aapishwa
(CRI Online) Februari 05, 2024
Rais mpya wa Namibia, Nangolo Mbumba ameapishwa siku ya Jumapili jioni kuwa rais wa nne wa taifa hilo baada ya rais wa nchi hiyo, Hage Geingob kufariki mapema siku hiyo.
Kiongozi huyo aliyehudumu nafasi ya makamu wa rais chini ya Serikali ya Rais Geingob ameapishwa katika Ikulu ya nchi hiyo.
Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Rais Mbumba ametoa pongezi kwa mtangulizi wake akimtaja kuwa msanifu mkuu wa katiba na utawala wa Namibia.
Mbumba ameapishwa kuwa Rais wa Namibia na Jaji Mkuu wa nchi hiyo kwa mujibu wa Katiba ya Namibia na atakuwa Rais hadi pale uchaguzi mkuu utakapofanyika baadaye mwaka huu.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma