Chuo Kikuu cha Rwanda chafanya hafla ya kusherehekea Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China

(CRI Online) Februari 05, 2024

Hafla ya kiutamaduni ya kusherehekea Sikukuu ijayo ya mwaka mpya wa jadi wa China wa dragoni imefanyika mjini Kigali, Rwanda.

Hafla hiyo imefanyika katika Taasisi ya Confucius iliyoko katika Chuo Kikuu cha Rwanda, na wengi walioshiriki ni wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kichina kwenye taasisi hiyo.

Shughuli zilizofanyika kwenye hafla hiyo ni pamoja na mhadhara unaoeleza Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, sanaa ya ukataji wa karatasi, na kuandika maneno ya Kichina yanayomaanisha baraka na furaha.

Mkurugenzi wa China kwenye Taasisi ya Confucius Zeng Guangyu amesema hafla hiyo inalenga kufundisha wanafunzi utamaduni wa China na kuwafanya wahisi mazingira ya mwaka mpya wa jadi wa China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha