Kuhisi msisimko wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwenye soko la Mwaka Mpya la Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 05, 2024

Kadiri Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China inavyowadia, ndivyo Wachina wanavyoanza kununua vyakula na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya sherehe ya sikukuu yao kubwa zaidi baada ya kufanya kazi katika mwaka mmoja unaokaribia kupita. Miaka minne tangu waandishi wa People's Daily Online, Zhao Tong na Alvaro Lago kutembelea soko la Mwaka Mpya mjini Beijing, wameamua kwenda kutembelea tena ili kuona kama kuna bidhaa zozote mpya zinazoonekana sokoni mwaka huu.

Kuanzia Mwaka 2024, sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China imechukuliwa kuwa siku rasmi ya mapumziko ya Umoja wa Mataifa katika kalenda yake ya mikutano. Pamoja na kuwa ni sherehe ya kila mwaka kwa watu wa China, Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China pia ni ya Dunia.

Fuata People's Daily Online na uhisi msisimko wa sherehe ya kimataifa yenye furaha na ustawi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha