Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Norway wafanya mazungumzo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 06, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide mjini Beijing, China, Februari 5, 2024. (Xinhua/ Yue Yuewei)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide mjini Beijing, China, Februari 5, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING- Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide mjini Beijing siku ya Jumatatu ambapo amesema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Norway, na uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekomaa na kuwa himilivu zaidi.

China inathamini serikali ya Norway kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na urafiki wake na China, amesema Wang ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China huku akiongeza kuwa ili kuhimiza maendeleo zaidi ya uhusiano kati ya China na Norway katika hatua inayofuata, pande zote mbili zinapaswa kushikilia njia sahihi ya kutendeana, kuendeleza kwa kina ushirikiano wenye matokeo halisi na kuimarisha uratibu wa pande nyingi.

Kwa upande wake Eide amesema, Norway inafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, inatetea maendeleo zaidi ya uhusiano wa pande mbili kwa kupitia mazungumzo ya kiujenzi na kujenga kwa pamoja Dunia ambayo ni ya jumuishi, yenye amani, ustawi na kupata maendeleo kwa pamoja.

Amesema upande wa Norway unathamini mageuzi ya China ya mtindo wake wa kupata ongezeko la uchumi, na Norway ingependa kushirikiana na China katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na changamoto nyingine za dunia nzima.

Pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni kwa kina kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide mjini Beijing, China, Februari 5, 2024. (Xinhua/ Yue Yuewei)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide mjini Beijing, China, Februari 5, 2024. (Xinhua/ Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha