China yaimarisha juhudi za utoaji wa mahitaji muhimu wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 06, 2024

Mtoto akiangalia midoli ya sikukuu kwenye supamaketi katika Wilaya ya Cengong, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Januari 23, 2024. (Picha na Tang Peng/Xinhua)

Mtoto akiangalia midoli ya sikukuu kwenye supamaketi katika Wilaya ya Cengong, Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Januari 23, 2024. (Picha na Tang Peng/Xinhua)

BEIJING – China imeongeza juhudi za kuhakikisha utoaji wa kutosha wa mahitaji muhimu wakati wa likizo ijayo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, Wizara ya Biashara ya China (MOC) imesema Jumatatu ambapo hatua zilizochukuliwa zinahusisha kuimarisha vyanzo vya bidhaa ili kuhakikisha kuwa zinapatikana kwa kutosha, nakusambazwa sokoni kwa wakati.

Juhudi pia zinaendelea ili kurahisisha uchukuzi na usambazaji ili bidhaa muhimu ziweze kufikiwa na watumiaji, wizara hiyo imesema.

Takwimu mpya za wizara hiyo zinaonyesha kuwa usambazaji wa mahitaji muhimu umeendelea kuwa wa kutosha nchi nzima na akiba ya bidhaa katika supamaketi kama vile nafaka, mafuta ya kupikia, nyama na mayai katika miji mikubwa 36 imeongezeka kwa asilimia 10 hadi asilimia 20 ikilinganishwa na mwanzo wa mwaka huu.

Likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China itaanza Februari 10 hadi 17 mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha