Lugha Nyingine
Kasri la Kifalme la Buckingham latangaza Mfalme Charles III wa Uingereza kugunduliwa kuwa na saratani
Mfalme Charles III wa Uingereza akitembelea kijiji cha Transylvanian cha Viscri, katikati mwa Romania, Juni 6, 2023. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)
LONDON - Mfalme Charles III wa Uingereza amegundulika kuwa na saratani na ameanza kupokea matibabu, Kasri la Kifalme la Buckingham limetangaza siku ya Jumatatu likisema aligundulika muda mfupi baada ya mfalme huyo mwenye umri wa miaka 75 kutibiwa tatizo la kupanuka kwa tezi dume.
"Mfalme alikuwa akitibiwa tatizo la kupanuka kwa tezi dume. Ilikuwa wakati wa matibabu hayo ambapo suala tofauti la wasiwasi lilibainishwa na baadaye kuthibitisha kuwa ni saratani," msemaji wa Kasri hilo amesema.
Taarifa kutoka kwenye kasri hilo imesema Mfalme "leo (Jumatatu kwa saa za Uingereza) ameanza ratiba ya matibabu ya kawaida, ambapo katika wakati huu ameshauriwa na madaktari kuahirisha kazi zinazohusu umma."
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika kipindi chote hicho, Mfalme ataendelea "kushughulikia kazi za nchi na zinazohusu nyaraka kama kawaida."
Picha ya Kasri la Kifalme la Buckingham jijini London, Uingereza, Julai 19, 2022. (Picha na Tim Ireland/Xinhua)
Mfalme "kwa ujumla anaendelea kuwa chanya juu ya matibabu yake na anatazamia kurudi kikamilifu katika majukumu ya umma haraka iwezekanavyo," imesema.
"Mfalme amechagua kuweka wazi ugonjwa wake ili kuzuia uvumi na kwa matumaini kwamba inaweza kusaidia uelewa wa umma kwa wale ambao wameathiriwa na saratani duniani kote," imeongeza.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ametoa taarifa akisema anamtakia mfalme kupona kabisa mapema iwezekanavyo.
“Sina shaka atarejea kwa nguvu zote muda si mrefu na najua nchi nzima itakuwa ikimtakia heri,” amesema.
Mfalme Charles wa III alisafiri kutoka Sandringham huko Norfolk hadi London Jumatatu asubuhi kuanza matibabu kama mgonjwa wa kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Mfalme wa Uingereza Charles III akiondoka kutoka kwenye Kasri la Kifalme la Buckingham kwa ajili ya kutawazwa kwake katika eneo la Westminster Abbey mjini London, Uingereza, Mei 6, 2023.(Xinhua/Li Ying)
Balozi: China imejikita katika kuendeleza uhusiano wa pande mbili na Ethiopia
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma