

Lugha Nyingine
Reli ya SGR ya Kenya yaongeza mabehewa mapya 50
Huduma ya uchukuzi ya reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi nchini Kenya imeongeza mabehewa mapya 50 ambayo yameagizwa kutoka China, ili kuboresha ufanisi wa huduma za reli nchini humo na kusaidia kuhamisha mizigo kutoka barabarani, na kupunguza uharibifu unaosababishwa na malori makubwa.
Katika taarifa iliyotolewa huko Mombasa, Kenya, Waziri wa Barabara na Uchukuzi Kipchumba Murkomen amesema kuwa mabehewa hayo mapya ni sehemu ya mwitikio wa kimkakati wa Kenya kwa mienendo ya soko, na haja ya kukidhi mahitaji yanayobadilika kila wakati ya wateja na kuongeza makali ya ushindani katika kanda.
Amebainisha kuwa hii ni mara ya kwanza kwa mabehewa mapya kuongezwa tangu kuzinduliwa kwa reli hiyo ya SGR Mei 2017, na kwamba shehena ya pili ya mabehewa 250 kutoka China inatarajiwa kuwasili baadaye Februari nchini humo.
Ameongeza kuwa mabehewa 20 kati ya hayo yanayotarajiwa kuletwa yatakuwa na plagi za umeme ili kuwezesha usafirishaji wa makontena yenye majokofu, biashara ambayo haijawahi kutumiwa hadi sasa kwa SGR.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma