Huduma za usafiri wa Barabara Kuu na reli zarejea kawaida hatua kwa hatua katika mikoa iliyokumbwa na theluji kubwa nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 07, 2024

Wafanyakazi wakijiandaa kufanya kazi kubwa ya kuondoa barafu kwenye daraja la Tianxingzhou juu ya Mto Yangtze huko Wuhan, Mkoa wa Hubei, katikati ya China, Februari 4, 2024. (Xinhua/Xiao Yijiu)

Wafanyakazi wakijiandaa kufanya kazi kubwa ya kuondoa barafu kwenye daraja la Tianxingzhou juu ya Mto Yangtze huko Wuhan, Mkoa wa Hubei, katikati ya China, Februari 4, 2024. (Xinhua/Xiao Yijiu)

WUHAN/CHANGSHA - Mkoa wa Hubei katikati mwa China uliokumbwa na hali ya kuanguka kwa theluji kubwa umesema siku ya Jumanne kwamba kuvurugika kwa ratiba za usafiri wa barabara kuu kulikosababishwa na barafu kulikuwa kunatarajiwa kutatuliwa Jumanne, baada ya vyombo vya usafiri kuanza kupita tena kwenye barabara kuu katika mkoa huo.

Barabara Kuu kote nchini China zimejaa magari huku kukiwa na pilika nyingi za watu kusafiri wakati wa sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China itakayoanzia Jumamosi, Februari 10.

Ingawa foleni kubwa za magari wakati wa sikukuu hiyo ni hali ya kawaida, mwaka huu zimeambatana na kunyesha kwa mvua ya barafu, kuanguka kwa theluji na hali ya barafu barabarani, ambayo yamekumba maeneo 18 ya ngazi ya kimkoa ya mashariki na katikati nchini China kuanzia Januari 31 hadi Februari 5.

Kwa kukabiliana na hali hiyo mbaya ya hewa, mamlaka za serikali za mitaa zimechukua hatua mbalimbali na mwitikio wa dharura.

Kundi la Kampuni za Shirika la Reli la China, Tawi la Wuhan Jumanne lilikuwa limepanga kutoa huduma 528 za treni, kuwaelekeza abiria waliokwama kutokana na kusimamishwa kwa huduma ya treni hapo awali ili kukabiliana na hali ya dharura ya malundo ya barafu kwenye stesheni za reli na kuhatarisha shughuli za treni.

Utabiri wa kituo cha hali ya hewa cha mkoa huo unaonesha kuwa mvua ya barafu na kuanguka kwa theluji kutaendelea katika mkoa huo katika siku mbili zijazo, na kutoa athari kwenye barabara kuu, reli na usafiri wa ndege.

Katika Mkoa jirani wa Hunan, wafanyakazi wamekuwa wakimwaga na kusambaza chumvi kwenye ardhi kujiandaa kwa kukabiliana na mvua ya barafu na kuanguka kwa theluji katika siku mbili zijazo.

Tangu Februari 1, mkoa huo umetuma maelfu ya watu katika timu 1,724, kusambaza vifaa vinavyoyeyusha theluji vyenye uzito wa tani 13,327, kufunga vifaa vyenye kuzuia kuteleza vya mita za ujazo 13,547 na mikeka 168,823 isiyoteleza barabarani.

"Tangu raundi ya hivi punde ya mvua na theluji, treni 198 zimefika salama, ingawa safari zilichelewa," amesema Ge Hui anayefanya kazi katika Kundi la Kampuni za Shirika la Reli la China, Tawi la Changsha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha