Eneo Maalum la Kiuchumi nchini Cambodia chini ya BRI larekodi ongezeko la biashara la asilimia 34.8 Mwaka 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 07, 2024

Picha hii iliyopigwa Mei 22, 2023 ikionyesha mandhari ya kiwanda cha Teknolojia ya Tairi cha General cha Cambodia katika Eneo Maalum la Kiuchumi la Sihanoukville (SSEZ) katika Mkoa wa Preah Sihanouk, Cambodia. (Picha na Ly Lay/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Mei 22, 2023 ikionyesha mandhari ya kiwanda cha Teknolojia ya Tairi cha General cha Cambodia katika Eneo Maalum la Kiuchumi la Sihanoukville (SSEZ) katika Mkoa wa Preah Sihanouk, Cambodia. (Picha na Ly Lay/Xinhua)

PHNOM PENH - Thamani ya uagizaji na uuzaji nje wa bidhaa kupitia Eneo Maalum la Kiuchumi la Sihanoukville (SSEZ) nchini Cambodia ilifikia dola za kimarekani bilioni 3.36 Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la mwaka hadi mwaka la asilimia 34.8, mwendeshaji wa eneo hilo amesema katika taarifa ya hivi majuzi.

Likiwekezwa kwa ubia na wawekezaji wa China na Cambodia, SSEZ ni mradi wa kinara chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI).

"Kiasi cha biashara kupitia SSEZ kilichangia asilimia takriban 7.18 ya jumla ya biashara ya Cambodia," imesema taarifa hiyo.

Eneo hilo maalum la kiuchumi lenye ukubwa wa kilomita za mraba 11 limevutia uwekezaji wenye thamani ya jumla ya dola bilioni 2.27 za kimarekani, likiwa na kampuni jumla ya 180 kutoka China, Ulaya, Marekani, Asia ya Kusini-Mashariki pamoja na nchi na kanda nyingine, na kutoa ajira 30,000 kwa wenyeji.

Sok Siphana, waziri mwandamizi na mwenyekiti wa heshima wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Maono ya Asia, amesema kuwa SSEZ, pamoja na miradi mingine mikuu ya BRI, imekuza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na muunganisho wa Cambodia.

"Ujenzi wa maeneo mbalimbali maalum ya viwanda kama vile Eneo Maalum la Kiuchumi la Sihanoukville, na ongezeko la mtaji na upanuzi wa uzalishaji wa matairi ya magari na mitambo ya kuzalisha saruji umeboresha kiwango cha maendeleo ya viwanda nchini Cambodia na kutoa idadi kubwa ya ajira na mapato ya ushuru kwa nchi," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi majuzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha