Erdogan atangaza mipango ya miundombinu huku baada ya mwaka mmoja tangu tetemeko la ardhi nchini humo kutokea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 07, 2024

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (katikati) akihudhuria hafla ya utoaji wa nyumba huko Kahramanmaras, Uturuki, Februari 6, 2024. (Picha na Mustafa Kaya/Xinhua)

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (katikati) akihudhuria hafla ya utoaji wa nyumba huko Kahramanmaras, Uturuki, Februari 6, 2024. (Picha na Mustafa Kaya/Xinhua)

ANKARA - Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza mipango mipya ya miundombinu siku ya Jumanne katika maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi ili kufanya kumbukumbu ya kutimia mwaka mmoja tangu kutokea kwa maafa hayo ambapo kwa mujibu wake kutakuwa na mradi mpya, ambao siyo tu utatoa makazi kwa wenyeji, lakini pia utasaidia shughuli za kiuchumi kwa kutoa fursa za ajira.

"Hatujengi tu nyumba, mitaa, au viwanja katika eneo la tetemeko la ardhi," amesema Erdogan, huku akitangaza kuanzishwa kwa mradi ambao utavutia uwekezaji kwenye sekta ya viwanda vya ulinzi katika majimbo yaliyoathiriwa na tetemeko hilo la ardhi.

"Tumezindua mradi wa nyumba na ajira ambao utaimarisha uwekezaji wa sekta ya viwanda vya ulinzi, sekta inayoongoza nchi yetu, katika miji yetu iliyokumbwa na tetemeko la ardhi. Kwa mipango iliyofanywa na Kurugenzi ya Sekta ya viwanda vya Ulinzi, tunajenga eneo la viwanda kwa Roketsan huko Kirikhan, Jimbo la Hatay. Tunaweka katika huduma kituo cha nyuzi za kaboni huko Gaziantep kwa usaidizi wa TUSAS (Kampuni za Anga ya Juu za Uturuki)," Erdogan amesema.

Serikali tayari imejenga kituo katika Jimbo la Kahramanmaras ili kuzalisha vifaa vya miundo ya vyombo vya safari ya anga kwa msaada wa TUSAS, Erdogan amesema.

"Sehemu nyingi za vyombo vya safari ya anga, zikiwemo za ndege yetu isiyoendeshwa na rubani ya Anka, zitazalishwa hapa kuanzia sasa. Kwa maneno mengine, tunaifanya Kahramanmaras kuwa kitovu chetu cha pili cha viwanda vya ulinzi, anga na anga ya juu baada ya Ankara," amesema Erdogan.

Mwaka mmoja uliopita, matetemeko mawili makubwa ya ardhi yalipiga kusini mwa Uturuki, na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 53,000 na kuacha maelfu ya watu bila makazi. Matetemeko hayo mawili ya ardhi yalikuwa maafa mabaya zaidi katika historia ya sasa ya Uturuki.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (katikati) akikabidhi funguo ya nyumba kwa mwanamke kwenye hafla ya utoaji wa nyumba huko Kahramanmaras, Uturuki, Februari 6, 2024. (Picha na Mustafa Kaya/Xinhua)

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (katikati) akikabidhi funguo ya nyumba kwa mwanamke kwenye hafla ya utoaji wa nyumba huko Kahramanmaras, Uturuki, Februari 6, 2024. (Picha na Mustafa Kaya/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha