Kundi la mwisho la mashine za kituo cha kuzalisha umeme kilichojengwa na China nchini Uganda launganishwa kwenye gridi ya kitaifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 07, 2024

Picha hii iliyopigwa Februari 6, 2024 ikionyesha vifaa vya Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji cha Karuma kilichojengwa na China huko Kiryandongo, Uganda. (Picha na Wang Jian/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Februari 6, 2024 ikionyesha vifaa vya Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji cha Karuma kilichojengwa na China huko Kiryandongo, Uganda. (Picha na Wang Jian/Xinhua)

KAMPALA - Uganda imefanikiwa kufunga kundi la mwisho la mashine sita katika Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji cha Karuma kilichojengwa na China na kuunganishwa kwenye gridi ya kitaifa, Kampuni ya Uzalishaji Umeme ya Uganda (UEGCL) imesema Jumanne.

Kampuni hiyo inayomilikiwa na serikali, imetoa taarifa kwenye Mtandao wa X, ambao zamani uliitwa Twitter, kwamba mashine hizo sita zinaweza kuzalisha umeme wenye nguvu za megawati 100 (MW), kimeunganishwa kwa mafanikio na gridi ya kitaifa Jumanne asubuhi.

"Hii inalifanya kuwa kundi la mwisho la mashine sita za kuzalisha umeme kufanyiwa majaribio yote kwa ajili ya uendeshaji," imeandika UEGCL.

Kampuni hiyo imesema kitengo cha kwanza cha kituo hicho kilikamilisha uendeshaji wake wa majaribio na majaribio ya kuunganishwa na gridi ya taifa Machi 21, 2023.

Wizara ya Nishati ya Uganda imesema, Kituo hicho cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji, kilichojengwa kwenye ardhi na chini ya ardhi katika sehemu ya chini ya Mto Nile Kaskazini mwa Uganda, kinatarajiwa kuzalisha umeme wenye nguvu za Megawati 600, huku kila mashine ikizalisha umeme wenye nguvu za Megawati 100.

Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji cha Karuma ni moja ya miradi kinara ya Uganda inayofadhiliwa na Benki ya Export-Import ya China, ambayo ilifadhili asilimia 85 ya gharama za mradi huo na asilimia 15 iliyobaki ilitoka kwa serikali ya Uganda.

Wataalamu husika wameeleza kuwa, kituo hicho ni muhimu katika kukidhi mahitaji ya umeme yanayoongezeka kwa kuharakisha maendeleo ya viwanda katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Karuma ni kituo cha pili cha kuzalisha umeme kufadhiliwa na China baada ya Kituo cha Kuzalisha Umeme wenye nguvu za Megawati 183 cha Bwawa la Isimba kilichoanza kufanya kazi Mwaka 2019. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha