Benki kuu ya Kenya yapandisha viwango vyake vya riba hadi asilimia 13 huku kukiwa na ongezeko la mfumuko wa bei

(CRI Online) Februari 07, 2024

Benki Kuu ya Kenya (CBK) Jumanne ilipandisha kiwango chake cha riba za mikopo hadi asilimia 13 kutoka asilimia 12.50 huku mfumuko wa bei ukiongezeka.

Katika taarifa yake iliyotolewa Nairobi, Gavana wa CBK, Kamau Thugge, ambaye aliongoza mkutano wa Kamati ya Sera ya Fedha (MPC), amebainisha kuwa mfumuko wa bei wa jumla umeendelea kuwa juu ya kiwango kilichowekwa.

Amesema kamati imeona kwamba vipengele vyote muhimu vya mfumuko wa bei yaani mafuta, chakula, na vitu visivyohusiana na chakula na mafuta (NFNF) vimeongezeka mwezi Januari.

Thugge ameongeza kuwa ongezeko la kiwango litahakikisha matarajio ya mfumuko wa bei yanaimarishwa na kushuka hadi asilimia 5.0 katikati ya kiwango kilichowekwa, pamoja na kushughulikia shinikizo lililobaki kwenye kiwango cha ubadilishaji fedha.

Nayo Benki Kuu ya Uganda (BoU), imetangaza kwamba itadumisha kiwango cha sera yake cha asilimia 9.5, ikitaja kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei kwa ufanisi. Katika taarifa yake ya sera ya fedha ya Februari, BoU imesema kuwa msimamo wa sera ya fedha unalingana na tathmini ya sasa ya mfumuko wa bei na matarajio ya ukuaji, ikiendelea kuunga mkono mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha