

Lugha Nyingine
Kiongozi wa Houthi nchini Yemen aapa kuongeza mashambulizi kama mgogoro wa Gaza utaendelea
Kundi la Houthi nchini Yemen limeapa kuongeza mashambulizi katika Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden kama mgogoro wa Gaza utaendelea.
Hayo yamo kwenye hotuba iliyotolewa Jumanne na kiongozi wa kundi hilo Abdul Malik al-Houthi kwenye kituo cha televisheni cha kundi hilo al-Masirah.
Amesema amezionya nchi za Marekani, Uingereza na Israel kwamba lazima ziache uvamizi wao na kuacha kuuzingira ukanda wa Gaza, la sivyo kundi hilo litaongeza mashambulizi zaidi.
Ametoa hotuba hiyo ili kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 tangu kuuawa kwa kaka yake mkubwa, Hussein Badreddin al-Houthi, ambaye ni mwanzilishi wa kundi hilo lenye silaha, na aliuawa wakati wa mapigano dhidi ya jeshi la serikali ya Yemen mwaka 2004 katika ngome ya Houthi kaskazini mwa Jimbo la Saada.
Mapema siku hiyo, kundi hilo lilidai kuhusika na mashambulizi dhidi ya meli ya jeshi la majini la Marekani na meli ya biashara ya Uingereza katika Bahari ya Shamu. Al-Houthi amebainisha kuwa kundi hilo liko tayari kuvuruga usafirishaji wa meli za kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma