Ushuhuda wa eneo la mradi wa uchimbuaji wa njia ya majini ya Bandari ya Dar es Salaam: Kuifanya bandari ya Tanzania kuwa ya kisasa zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 07, 2024

Meli ya uchimbuaji matope ya “Tongxu” iliyosanifiwa na kuundwa na China kwa kujitegemea ikifanya kazi ya kuchimbua matope kwenye Bandari ya Dar es Salaam, Tanzania.

Meli ya uchimbuaji matope ya “Tongxu” iliyosanifiwa na kuundwa na China kwa kujitegemea ikifanya kazi ya kuchimbua matope kwenye Bandari ya Dar es Salaam, Tanzania. (Picha na Bian Liang)

Wafanyakazi wa mradi wa kuchimbua matope kwenye njia ya majini ya Bandari ya Dar es Salaam wakibadilisha taa ya kuongoza meli za mnara katika Kisiwa cha Makatumbe.

Wafanyakazi wa mradi wa kuchimbua matope kwenye njia ya majini ya Bandari ya Dar es Salaam wakibadilisha taa ya kuongoza meli za mnara katika Kisiwa cha Makatumbe. (Picha na Guo Cuncang)

Bandari ya Dar es Salaam inajulikana kama “Bandari ya Lango” ya Tanzania, ikiwa ni kituo muhimu cha usafirishaji wa mizigo na cha biashara katika Afrika Mashariki. Mnamo Agosti 27, 2021, mradi wa uchimbuaji matope kwenye njia ya majini ya Bandari ya Dar es Salaam, ambao unatekelezwa na Kampuni ya Bandari ya China (CHEC) ulianza rasmi. Huu ni mradi muhimu wa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI)” unaojengwa kwa pamoja na nchi mbili za Tanzania na China.

Baada ya miaka zaidi ya miwili, mradi huo umeingia hatua ya mwisho. Wakati wa saa za mwisho mwisho kuelekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China, mwandishi wa habari wa People’s Daily alikwenda kwenye eneo la ujenzi wa mradi huo, kufanya mahojiano na kurekodi hamasa ya wajenzi wa nchi hizo mbili katika kujenga pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

“Kuinua zaidi kiwango cha kufungua mlango cha Tanzania na Afrika ya Mashariki”

Katika Kisiwa cha Makatumbe kilichopo Kaskazini Mashariki ya Bandari ya Dar es Salaam, wafanyakazi wa Tanzania na China walikuwa wakishirikiana kubadilisha taa za kuongoza meli kwenye mnara.

“Taa hizi za zamani za kuongoza meli zilikuwa katika hali ya uchakavu kwa miaka mingi, na rangi za mwanga na mawimbi ya ishara yalikuwa yameathiriwa, hali ambayo iliathiri uingiaji wa kawaida wa meli kwenye bandari.” Baada ya Mratibu wa mradi huo Salehe Nuhu na wenzake kumaliza kubadilisha taa, walifanya majaribio na marekibisho ya mwanga wa taa na kadhalika, hadi mawimbi ya ishara yalipotumwa kwa usahihi. Kazi kama hii ya kubadilisha taa pia itafanywa katika sehemu nyingine za bandari.

Mradi wa uchimbuaji kwenye njia ya majini ya Bandari ya Dar es Salaam unahusisha uchimbuaji wa matope, uibuaji na ukwamuaji wa meli zilizozama, ununuaji na ufungaji wa vifaa vya kuongoza na kusaidia meli. Kwa mujibu wa Mkuu wa mradi huo Bian Liang upanuaji wa njia ya majini ya bandari, uchimbuaji matope na kazi nyingine zimekamilika, na ufungaji na uwekaji wa minara katika ardhi na taa za minara unaendelea.

Foum, mshauri wa mradi huo amesema kuwa, Bandari ya Dar es Salaam ni nguzo muhimu ya maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Na kwamba baada ya mradi huo kukamilika utaimarisha na kuboresha nafasi ya bandari hiyo kama kituo muhimu cha kikanda cha usafirishaji wa majini, kuinua zaidi kiwango cha kufungua mlango cha Tanzania na Afrika ya Mashariki, na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa nchi jirani.

“Kuhimiza Ulinzi wa Mazingira ya asili na Bioanuwai za baharini”

Wakati wa mchakato wa kuchimbua njia ya baharini, timu ya mradi huo ilichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka vizuizi vya mafuta machafu, ili kuhakikisha maisha ya kawaida ya viumbe wa baharini na kupunguza kadri iwezavyo athari mbaya za mradi huo kwa mazingira ya asili.

Kulinda bioanuwai za baharini ni kipaumbele cha juu katika kazi za mradi huo. Katika eneo la mradi na maeneo mengine yanayouzunguka, timu ya mradi huo mara kwa mara hupima hali ya maji. “Rekodi saba za upimaji wa majini zinaonesha kuwa, idadi ya matumbawe hai kwenye eneo la ujenzi na maji yanayolizunguka imeongezeka kwa asilimia 15 ikilinganishwa na ile ya kabla ya mradi,” amesema Guo Zhenchuan, msimamizi mkuu wa mambo ya usalama wa mradi huo.

Amour ni mhandisi wa mazingira wa timu ya mradi huo. Kwa maoni yake, mashine zenye ubora wa juu na teknolojia za kampuni ya China zinahakikisha mchakato wa ujenzi kuwa wa kijani na wenye kulinda mazingira ya asili, “na kuhimiza ulinzi wa ikolojia ya mazingira na bioanuwai za baharini, na kufuata dhana ya maendeleo endelevu.”

“Ninatarajia sana kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China pamoja na wenzangu”

Salehe Nuhu amekuwa akifanya kazi kwa miaka mwili katika mradi huo wa uchimbuaji njia ya majini ya Bandari ya Dar es Salaam. Kwa sasa amekuwa mtu mwenye ujuzi wa mambo mbalimbali anayehusika na kazi ya uratibu na mawasiliano, kazi za ulinzi wa mazingira kwenye mradi na usimamizi wa wafanyakazi wenyeji.

Saleh amesema kuwa, wafanyakazi wenzake wa China “ni kama ndugu na walimu” na “hii ni timu bora kuwahi kufanya nayo kazi pamoja”.

Katika sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ya mwaka huu, wafanyakazi wa China na Tanzania watafanya pamoja sherehe kama vile kufumbana mafumbo kwenye taa. “Tunatazamia sana kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China pamoja na wenzetu wa China!”Saleh amesema huku akiongeza kuwa, ingawa wanatoka nchi tofauti, lakini Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China imekuwa sikukuu ya Kidunia. “Tutatumiana salamu za heri na kutakiana mema na kusherehekea pamoja sikukuu hiyo ya furaha na shamrashamra.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha