Makamu wa Rais wa Tanzania azitaka serikali za Afrika kushughulikia changamoto za ajira

(CRI Online) Februari 08, 2024

Makamu wa Rais wa Tanzania Philip Mpango amezitaka serikali za Afrika kukabiliana na changamoto zinazohusiana na utoaji wa nafasi za ajira, akisema zinahitajika mbinu jumuishi, za kimageuzi na shirikishi.

Akifungua Mkutano wa 7 wa Washirika wa Kijamii wa Afrika Jumatano jijini Dar es Salaam, Mpango amebainisha kuwa utoaji wa ajira na mikakati inayohimiza ukuaji wa kiuchumi na maendeleo shirikishi vimekuwa vipaumbele muhimu vya serikali zote za Afrika.

Ameongeza kuwa mikutano ya Kilele ya Washirika wa Kijamii ya Afrika imetoa maarifa na miongozo ya kuongeza fursa za ajira kote Afrika.

Mpango amesema changamoto za ajira barani Afrika zimechangiwa zaidi na msukosuko wa mabadiliko ya tabianchi duniani, athari mbaya za migogoro inayoendelea katika Bara la Afrika, athari za mivutano ya siasa za kijiografia katika maeneo kadhaa ya dunia, pamoja na athari mbaya za janga la UVIKO-19.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha