Rais Xi Jinping atoa salamu za mwaka mpya wa jadi kwa Wachina wote

(CRI Online) Februari 11, 2024

Kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la Serikali la China, Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za mwaka mpya wa jadi wa China kwa Wachina wote kwenye tafrija iliyofanyika Tarehe 8, Februari kwenye Jumba la Mikutano ya Umma hapa mjini Beijing.

Rais Xi amesema Mwaka wa Sungura ambao umemalizika, umekuwa mwanzo wa utekelezaji kamili wa mipango na maagizo ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China katika nyanja zote, akibainisha kuwa China inakabiliwa na mazingira yenye utata ya kimataifa na kazi ngumu za mageuzi, maendeleo na kudumisha utulivu.

Rais Xi ameongeza kuwa China imeunganisha nguvu pamoja kuelekea China yenye maendeleo ya mambo ya kisasa, huku ikizingatia mazingira ya ndani na ya kimataifa, kushinda taabu na changamoto nyingi, na kupiga hatua thabiti katika safari mpya ya kuijenga China kuwa nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya mambo ya kisasa kwa pande zote.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha