Tamasha kubwa la “Chunwan” lakaribisha mwaka mpya wa jadi wa China wa Dragoni

(CRI Online) Februari 11, 2024

Tarehe 9 Februari ilikuwa mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China wa Dragoni ambapo saa 2 usiku wa siku hiyo, likiambatana na nyimbo na ngoma mbalimbali, tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China ambalo huandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG limerushwa hewani.

Mwaka 1983, kituo cha taifa cha televisheni cha China (CCTV) kiliandaa tamasha la kwanza la sanaa na utamaduni la mwaka mpya wa jadi wa China , liitwalo “Chunwan”. Kila ifikapo mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China, wanafamilia kujumuika na kukaa pamoja kutazama tamasha hilo imekuwa ni desturi ya watu wa China.

Tamasha hilo la mwaka 2024 limejumuisha utamaduni wa jadi wa China, likitumia njia za kisasa za sanaa na uvumbuzi wa teknolojia mbalimbali za mwanga na kivuli. Pia limejumuisha maonesho ya nyimbo na ngoma, mazingaombwe, opera, wushu, sarakasi na vipindi vya aina mbalimbali.

Mbali na watu wa China, watu kutoka miji 90 ya nchi 49 duniani pia waliweza kutazama tamasha hilo moja kwa moja kupitia luninga zaidi ya 3000 zilizofungwa nje ya nyumba.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha