Rais wa Tanzania asema uchaguzi utakuwa huru na wa haki

(CRI Online) Februari 11, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema haki, demokrasia, sheria na utawala bora viutadumishwa kwa watu wote wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Rais Samia amesema hayo katika sherehe za kukaribisha mwaka mpya wa 2024 kwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu ya Tanzania.

Amesema, ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, Kikosi Kazi huru cha kupitia na kushauri mageuzi muhimu katika mfumo wa siasa kiliundwa na kuwasilisha ripoti yake mwaka 2023.

Rais Samia pia amesema mapendekezo mengi ya Kikosi Kazi hicho yaliyopokelewa na serikali na wadau wote yalihusu kuongeza uwazi katika michakato ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha