China yapinga na kulaani Israel kufanya mashambulizi katika eneo la Rafah

(CRI Online) Februari 14, 2024

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema kuwa China inatilia maanani sana hali ya eneo la Rafah. Pia ameeleza kuwa inapinga na kulaani vitendo vya kudhuru raia na kukiuka sheria za kimataifa, ambapo inaitaka Israel isimamishe operesheni za kijeshi haraka iwezekanavyo.

Amesema hayo wakati akijibu maswali ya wanahabari waliotaka kujua China ina maoni gani kuhusu mashambulizi makubwa ya anga yaliyofanywa na jeshi la Israel katika eneo la Rafah kusini mwa Gaza ambayo yamesababisha vifo na majeruhi.

Msemaji huyo pia amebainisha kuwa China inaitaka Israel ifanye kila juhudi kuepusha madhara kwa raia wasio na hatia, na kuzuia maafa makubwa zaidi ya kibinadamu katika eneo la Rafah.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha