Watanzania watoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa

(CRI Online) Februari 14, 2024

Mamia ya Watanzania jana walitoa heshima zao za mwisho kwa waziri mkuu wao wa zamani Bw. Edward Lowassa, aliyefariki Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mrefu akiwa na umri wa miaka 70.

Mwili wa Bw. Lowassa uliagwa katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es Salaam huku mtu mmoja baada ya mwingine akitoa heshima za mwisho kwa Bw. Lowassa aliyefariki katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Siku ya Jumapili, waziri mkuu wa Tanzania Bw. Majaliwa alitangaza kuwa Bw. Lowassa atazikwa kijijini kwao Ngarash wilayani Monduli mkoani Arusha Februari 17, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan atahudhuria mazishi yake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha