

Lugha Nyingine
Naibu Waziri Mkuu wa DRC asema jeshi la taifa na MONUSCO wanapambana na M23 kwa pamoja
(CRI Online) Februari 14, 2024
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jean-Pierre Bemba amesema Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) kinashirikana na kikosi cha jeshi la taifa la DRC FARDC katika kupambana dhidi ya kundi la waasi la M23 mashariki mwa nchi hiyo, licha ya kuendelea na mchakato wa kujiondoa kwake.
Bemba ameyasema hayo Jumanne mjini Goma, Jimbo la Kivu Kaskazini, ambako hali ya wasiwasi imeongezeka kutokana na mapigano makali kati ya jeshi la taifa la DRC na kundi la M23 katika mji wa Sake na maeneo ya karibu, umbali wa takriban kilomita 23 kaskazini magharibi mwa Goma.
Ufafanuzi huo unalenga kusahihisha uvumi kwamba MONUSCO na M23 wanashirikiana pamoja.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma