Xi Jinping apongeza Mkutano wa 37 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 18, 2024

Rais Xi Jinping wa China tarehe 17 alituma salamu za pongezi kwa Mkutano wa 37 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika.

Xi alisema, hivi sasa dunia inakabiliana na mabadiliko yasiyotokea katika miaka 100 iliyopita, ambapo nchi za Kusini ya Dunia zinazowakilishwa na China na nchi za Afrika zinapata maendeleo ya kasi, na kuleta uhimizaji kwa kina mchakato wa historia ya Dunia. Umoja wa Afrika unashikamanisha nchi za Afrika na kuzifanya zijipatie maendeleo, na kusukuma mbele kwa nguvu kubwa umoja wa ukanda huo na ujenzi wa eneo la biashara huria. Umoja wa Afrika umejiunga na kundi la G20 kwa mafanikio, hali ambayo imewezesha Afrika kuongeza tena uwakilishi wake na ushawishi wake katika usimamizi wa Dunia nzima. Upande wa China unapongeza kwa udhati mafanikio hayo yote.

Xi alisisitiza kuwa, katika mwaka uliopita, uhusiano kati ya China na Afrika umendelezwa kwa kina, ambapo mkutano kati ya viongozi wao umefanyika kwa mafanikio, na pande hizo mbili zimeamua kuungana mkono katika utafutaji wa njia za kupata maendeleo ya kisasa, na kujenga pamoja mazingira mazuri ili kutimiza ndoto ya maendeleo. Mkutano mwingine wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afirka (FOCAC) utafanyika mwaka 2024, na Xi amesema, angependa kushirikiana na viongozi wa Afrika katika kuweka mkazo katika kuleta manufaa kwa watu wa pande hizo mbili, kupanga kwa makini mpango mpya wa ushirikiano wa China na Afrika, na kusukuma mbele ujenzi wa pamoja wa jumuiya ya China na Afrika ya kiwango cha juu yenye mustakabali wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha