Watetezi wa kanuni ya kuwepo kwa China moja wanapaswa kuunga mkono Muungano wa Taifa wa amani kwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 19, 2024

MUNICH - Wale wanaoshikilia na kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja wanapaswa kuunga mkono Muungano wa Taifa wa amani kwa China, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema katika Mkutano wa 60 wa Usalama wa Munich alipokuwa akijibu swali linalohusiana na Taiwan baada ya kutoa hotuba yake kuu katika mjadala wa "China Duniani" kwenye mkutano huo.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesisitiza kuwa Taiwan ni sehemu ya China siku zote.

Mnamo Mwaka 1943, serikali za China, Marekani na Uingereza kwa pamoja zilitoa Azimio la Cairo, ambalo linaeleza wazi kwamba maeneo yote ambayo Japan ilikuwa imeyaiba kutoka kwa Wachina, kama vile Taiwan, yatarejeshwa kwa China, Wang amebainisha, huku akiongeza kuwa Ibara ya 8 ya Tamko la Potsdam lililotolewa Mwaka 1945 linaeleza kuwa masharti ya Azimio la Cairo yatatekelezwa.

“Nyaraka za Umoja wa Mataifa pia zimeeleza waziwazi kuwa Taiwan ni Mkoa wa China,” ameongeza Wang huku akisisitiza kwamba mambo yote haya yamedhihirisha vya kutosha kwamba suala la Taiwan kwa asilimia mia moja ni mambo ya ndani ya China.

Taiwan haijawahi na haitakuwa nchi, Wang amesema, huku akibainisha kuwa huu ni ukweli wa kihistoria na makubaliano ya jumuiya ya kimataifa.

Likiwa suala lililobaki ambalo bado halijatatuliwa tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China, Taiwan hatimaye itarejea katika kukumbatia nchi mama na pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan hakika zitafanikiwa kuungana tena, amesema Wang.

"Ni nia thabiti ya watu bilioni 1.4 wa China na mwelekeo usioepukika wa historia," ameongeza.

Ili kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja, nchi zinapaswa kuunga mkono Muungano wa Taifa wa amani kwa China, na kudumisha amani na utulivu katika eneo la Mlango-Bahari wa Taiwan, ni lazima kupinga "kujitenga kwa Taiwan," amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha