Soko la utalii la China lastawi sana wakati wa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 19, 2024

Watalii wakitembelea eneo la kivutio la Hekalu la Fuzi (Confucius) huko Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Februari 14, 2024. Wachina wengi zaidi siku hizi wanachagua safari za utalii wakati wa sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ili kujionea tamaduni tofauti na hali ya mwaka mpya wa jadi wa China. (Picha na Su Yang/Xinhua)

BEIJING - China imeshuhudia safari milioni 474 za watalii ndani ya nchi wakati wa likizo ya siku nane ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China iliyomalizika Jumamosi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 34.3 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya nchi hiyo Jumapili.

Matumizi ya watalii katika safari zao za ndani ya nchi imefikia Yuan karibu bilioni 632.7 (kama dola za Kimarekani bilioni 89.07) , ikiwa ni ongezeko la asilimia 47.3 mwaka hadi mwaka, takwimu hizo zimeonyesha.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, China Bara imeshuhudia watalii milioni 3.6 wakisafiri nje ya nchi na watalii milioni 3.23 wakiwasili katika likizo hiyo ya siku nane, wakati ambapo sera nzuri kama vile kusameheana viza baina ya nchi zimeongeza kasi ya kuimarika kwa masoko ya utalii wa kimataifa.

Wakati wa likizo hiyo, maonyesho ya sanaa na burudani ya kibiashara 16,300 yalifanyika kote nchini China, mauzo ya tiketi yamefikia yuan milioni 778, ambayo ni ongezeko la asilimia 52.1 na asilimia 80.09 mwaka hadi mwaka, mtawalia. Maonyesho hayo yalivutia watazamaji zaidi ya milioni 6.57, ikiwa ni ongezeko la mwaka hadi mwaka la asilimia 77.71, kwa mujibu wa wizara hiyo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha