

Lugha Nyingine
Rais wa Mauritania achukua nafasi ya uenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika
(CRI Online) Februari 19, 2024
Rais Mohamed Ould Cheikh Ghazouani wa Mauritania amechukua nafasi ya uenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika (AU) katika ufunguzi wa Mkutano wa 37 wa Kawaida wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Afrika, kutoka kwa mwenyekiti wa Umoja huo anayemaliza muda wake, Rais Azali Assoumani wa Visiwa vya Comoro.
Kwenye hotuba yake Rais Mohamed Ould Cheikh Ghazouani amesisitiza haja ya kutambua matarajio ya waasisi wa Umoja wa Afrika, hasa ya uhuru wa kijamii na kiuchumi, umoja na ustawi wa Afrika.
Bwana Azali Assoumani amesema katika kipindi chake aliangazia masuala muhimu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uthabiti na maendeleo ya Afrika, kuinua nafasi ya Afrika kwa ujumla katika hatua za kimataifa, pamoja na mageuzi ya jumuiya hiyo yenye wanachama 55.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma