Mkutano wa kilele wa AU wataka kuwepo mshikamano wa kimataifa kwa Palestina

(CRI Online) Februari 19, 2024

(Picha inatoka cri)

(Picha inatoka cri)

Viongozi wa Afrika Jumamosi walihimiza "kukomeshwa mara moja" kwa mgogoro wa Palestina na Israel, wakitoa wito wa kuwepo mshikamano wa kimataifa kwa Palestina wakati wa mkutano wa 37 wa Umoja wa Afrika (AU).

Akiongea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 37 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU, Mwenyekiti wa AU wa mwaka 2024 ambaye pia ni Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Cheikh Ghazouani, amesema hali ya sasa ya Gaza ni kielelezo dhahiri cha umuhimu wa mageuzi ndani ya mfumo wa kimataifa ulio na dhuluma kubwa na viwango vinavyotofautiana.

Amewaambia viongozi wa Afrika kuwa ni muhimu kutambua haki ya asili ya Wapalestina ya kuanzisha taifa lao huru, na Jerusalem Mashariki ukiwa mji mkuu wake, kwa kuzingatia maazimio muhimu halali ya kimataifa.

Pia ameelezea wasiwasi wake juu ya kusitasita kwa jumuiya ya kimataifa kutoa ushawishi unaohitajika kwa ajili ya usimamishaji wa mapigano mara moja, kutoa misaada, na kuanzishwa kwa suluhu ya pande zote na ya kudumu.

Naye Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Moussa Faki Mahamat, pia amesisitiza haja ya dharura ya kushughulikia suala la Palestina.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha