China, Marekani zakubaliana kutekeleza makubaliano ya mkutano wa wakuu wa nchi hizo mbili wa San Francisco

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 20, 2024

Mjumbe wa Baraza la Serikali la China ambaye pia ni Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong akikutana na Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Alejandro Mayorkas mjini Vienna, Austria, Februari 18, 2024. (Xinhua)

Mjumbe wa Baraza la Serikali la China ambaye pia ni Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong akikutana na Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Alejandro Mayorkas mjini Vienna, Austria, Februari 18, 2024. (Xinhua)

VIENNA - Mjumbe wa Baraza la Serikali la China ambaye pia ni Waziri wa Usalama wa Umma wa China, Wang Xiaohong na Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Alejandro Mayorkas Jumapili walikutana huko Vienna, ambapo wamekubaliana kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa katika mkutano wa San Francisco kati ya wakuu wa nchi hizo mbili.

Maafisa hao wawili walikuwa na mawasiliano ya dhati, ya kina na ya kiujenzi juu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa San Francisco kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, kuendeleza ushirikiano wa pande mbili katika udhibiti wa dawa za kulevya na utekelezaji wa sheria, na kushughulikia masuala yanayofuatiliwa na kila upande.

Wang amesema Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Marekani Joe Biden waliweka wazi "Maono ya San Francisco" yenye mwelekeo wa siku za baadaye walipokutana mjini San Francisco.

Wang amesema anatumai kuwa pande hizo mbili zitazingatia maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu hao wawili, kushikilia kanuni za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kushirikiana kwa kunufaishana, kuheshimu maslahi ya msingi na masuala yanayofuatiliwa na kila upande, na kuondoa vikwazo katika ushirikiano wa pande mbili katika kudhibiti dawa za kulevya na kutekeleza sheria na mawasiliano kati ya watu.

Wang huku akitoa wito kwa Marekani kuhakikisha usalama wa ujumbe wa kidiplomasia na kibalozi na wafanyakazi wa China nchini Marekani, kuondoa vizuizi vya visa kwa taasisi husika na wafanyakazi wa China nchini Marekani, ameitaka Marekani iache kunyanyasa na kuhoji wanafunzi wa China bila sababu, na kuhakikisha kuwa raia wa China wana haki ya kuingia nchini humo na kupata heshima kamili.

Pande hizo mbili zimekubaliana kuchangia katika maendeleo thabiti ya uhusiano kati ya China na Marekani kwa kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kudumisha mazungumzo na ushirikiano juu ya udhibiti wa dawa za kulevya na utekelezaji wa sheria, kuweka umuhimu kwa masuala yanayofuatiliwa na kila upande, na kutatua masuala ipasavyo kwa msingi wa kuheshimiana, kudhibiti tofauti na kushirikiana kwa kunufaishana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha