Mkutano wa kilele wa 37 wa AU wamalizika kwa kuainisha vipaumbele vya Afrika vya Mwaka 2024 na baadaye

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 20, 2024

ADDIS ABABA- Mkutano wa 37 wa Kawaida wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) umehitimishwa Jumapili kwa kuainisha vipaumbele vya Afrika vya mwaka 2024 na siku za baadaye.

Mkutano huo wa siku mbili, uliowaleta pamoja viongozi wa Afrika kutoka nchi wanachama wa AU katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, umefanyika chini ya kaulimbiu ya AU ya mwaka 2024 "Elimisha Mwafrika anayefaa kwa Karne ya 21: Kujenga mifumo thabiti ya elimu kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa elilmu jumuishi, kwa maisha yote, yenye ubora na inayofaa Afrika."

Wakati Bara la Afrika likiangazia elimu katika Mwaka 2024, mkutano huo umejadili jinsi inavyoimarisha elimu na ujuzi ili kukidhi dira ya bara hilo na mahitaji ya soko.

Pamoja na kujadili juu ya maendeleo, changamoto na matarajio ya maendeleo ya jumla ya Afrika, viongozi wa Afrika waliohudhuria mkutano huo wamejadili vipaumbele muhimu vya bara hilo kutoka amani na usalama hadi mabadiliko ya tabianchi, maendeleo ya kiuchumi na umuhimu wa Afrika katika muktadha mpana wa kimataifa wa pande nyingi.

Mkutano huo pia umeshuhudia kuchaguliwa kwa Mohamed Ould Cheikh Ghazouani, Rais wa Mauritania, kuwa mwenyekiti wa zamu wa AU kwa Mwaka 2024, akichukua zamu kutoka kwa Azali Assoumani, Rais wa Comoro.

Assoumani, ambaye aliwasilisha ripoti ya kina kuhusu mafanikio na shughuli zilizofanywa na AU, amebainisha mafanikio katika amani na usalama, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, uwezeshaji wa vijana na wanawake, na Afrika kutoa sauti moja na kuchukua misimamo ya pamoja kuhusu masuala ya kimataifa, miongoni mwa mengine.

Mkutano huo, ambao ni chombo cha juu zaidi cha kufanya maamuzi cha AU, umeangazia mafanikio na mapungufu yaliyobainishwa katika muongo wa kwanza wa utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa Bara la Afrika wa miaka 50, wa Ajenda ya 2063.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha