

Lugha Nyingine
Ushirikiano kati ya China na Afrika wapongezwa kwenye Mkutano wa 37 wa wakuu wa nchi za AU
NAIROBI – Rais wa China Xi Jinping alituma salamu za pongezi kwa Mkutano wa 37 wa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) siku ya Jumamosi, akitoa wito wa kuweka dira mpya kwa ushirikiano wa China na Afrika, na kuhimiza ujenzi wa pamoja wa jumuiya ya kiwango cha juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
Wadau wa nchi za Afrika kutoka sekta mbalimbali wamesema wanathamini ujumbe wa Xi, wakiamini kuwa unaonesha utiaji maanani wa China kwa Afrika na uungaji mkono wake thabiti katika maendeleo ya bara hilo.
Wanaamini kwamba uhusiano wa China na Afrika utaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano wa Kusini-Kusini, wakitarajia kufanya juhudi pamoja kwa ajili ya kupata maendeleo ya kisasa.
“Ujumbe wa Rais Xi unadhihirisha dhahiri kuwa China iko upande wa Afrika katika juhudi zake za maendeleo,” amesema Lalu Etalla, mhariri mwandamizi wa Shirika la Utangazaji la Ethiopia.
Mwaka jana, uingiaji wa Ethiopia katika kundi la BRICS na uanachama rasmi wa Umoja wa Afrika katika Kundi la 20 (G20) vyote viliungwa mkono na China kwa kiasi kikubwa, amesema Etalla, akisisitiza kuwa hali hiyo inawakilisha ushindi muhimu kwa ushirikiano wa Kusini-Kusini na inabeba ushindi muhimu kwa ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea, kupaza sauti zao katika jukwaa la Dunia.
Youssouf Mandoha Assoumani, Mwenyekiti wa Kamati ya Wajumbe wa Kudumu ya AU, ametoa shukrani zake kwa juhudi na mchango wa China wa pande zote katika maendeleo ya bara hilo.
“Afrika inatambua na itaendelea kustawisha ushirikiano huu wa manufaa kwa pande zote baina ya pande hizo mbili, vilevile uwenzi wa mfano wa kuigwa,” amesema Assoumani.
Benjamin Mgana, mhariri mkuu wa gazeti la The Guardian la Tanzania, amesema kuwa ujumbe wa Xi unasisitiza umuhimu wa mshikamano na umoja kati ya nchi za Afrika, na pia unasitiza nafasi ya Afrika katika uongozi wa Dunia, ikionesha uungaji mkono imara wa China kwa maendeleo ya Afrika na kujitolea kwake kuimarisha ushirikiano.
“Ninaamini kuwa uzoefu wa maendelo wa China ni wenye manufaa siyo tu kwa Afrika lakini pia kwa nchi nyingine zinazoendelea,” amesema Raissa Ada Allogo, ofisa mwandamizi wa sera wa Idara ya Maendeleo ya Miundombinu na Nishati ya Umoja wa Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma