Lugha Nyingine
Ofisa wa Umoja wa Afrika asema Ushirikiano na China katika sekta za elimu, mafunzo ya ufundi stadi ni muhimu kwa maendeleo ya rasilimali watu barani Afrika
Kamishna wa Umoja wa Afrika (AU) wa Maendeleo ya Kiuchumi, Biashara, Utalii, Viwanda na Madini, Bw. Albert Muchanga amesema ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi ni "muhimu sana" na huwezesha maendeleo ya rasilimali watu.
Bw. Muchanga amesema ana matarajio makubwa kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya China na Afrika katika sekta hiyo, na kuishukuru China katika kuisaidia Afrika kuendeleza vipaji.
Bw. Muchanga amesema China na Afrika zinashirikiana vizuri na kuna mazungumzo endelevu na kuna mifumo ya ushirikiano katika sekta ya elimu. Pia amesema kuna wanafunzi wengi wa Afrika wanaonufaika kupitia ufadhili wa masomo, na kuwa ahadi zilizotolewa na serikali ya China hivi karibuni kwa Afrika zitaimarisha uungaji mkono kwa nchi za Afrika katika kukuza vipaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



