Tanzania yachaguliwa tena kuwa mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika

(CRI Online) Februari 20, 2024

Tanzania imechaguliwa tena kuwa mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC) kwa muda wa miaka miwili kuanzia Aprili mosi mwaka huu.

PSC ilitoa taarifa kuhusu uchaguzi huu siku ya Alhamisi kupitia Mtandao wa X, zamani Twitter, na pia kutaja wajumbe wengine tisa waliochaguliwa kuwa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Guinea ya Ikweta, Uganda, Misri, Angola, Botswana, Cote d'Ivoire, Sierra Leone na Gambia.

PSC ni chombo cha kudumu cha kufanya maamuzi cha AU kwa ajili ya kuzuia, kusimamia na kutatua migogoro.

Baada ya Tanzania kuchaguliwa tena, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania January Makamba, aliandika tena kwenye mtandao wa X taarifa za Umoja wa Afrika na kuwashukuru walioipigia kura Tanzania.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha