Kujihami kiuchumi kwa Marekani na Ulaya dhidi ya sekta ya magari ya China kutaumiza maendeleo yao ya muda mrefu: msemaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2024

BEIJING - Hatua za kujihami kibiashara zinazochukuliwa na Marekani na Ulaya zitaathiri maendeleo yao ya muda mrefu na maendeleo na ustawi wa Dunia, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema mjini Beijing siku ya Jumanne.

Imeripotiwa kuwa Marekani inafikiria kuzuia uagizaji wa magari ya teknolojia za kisasa ya China na vifaa vinavyohusika kwa njia zisizo za ushuru. Umoja wa Ulaya (EU) umeanzisha uchunguzi wa dhidi ya ruzuku katika uagizaji wa magari yanayotumia nishati ya umeme kutoka China.

Katika kujibu hatua hizo, Mao Ning amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba mgawanyo wa majukumu na ushirikiano wa kunufaishana ni sifa za kipekee za mnyororo wa viwanda vya magari.

"Maendeleo ya sekta ya magari ya China yametoa bidhaa za gharama nafuu na zenye ubora wa hali ya juu duniani," amesema, huku akiongeza kuwa kila gari moja kati ya matatu yanayosafirishwa nje ya nchi kutoka China ni gari linalotumia nishati ya umeme, hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa katika mabadilishaji ya muundo wa uchumi wa kijani na wenye utoaji kaboni chache.

Mao amesema kama Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alivyosema, hatua za kujihami kibiashara zinazochukuliwa na nchi husika dhidi ya China, kugeuza shughuli za kawaida za biashara kuwa masuala ya usalama na itikadi, kujenga "ua ndogo zilizo na uzio mrefu" kwa jina la "kuondoa hatari" na jaribio la "kuwaangusha wengine" badala ya "kukimbia kwa kasi" inaweza kuonekana kama ushindi, lakini kwa kweli ni hasara kwa maendeleo ya muda mrefu ya nchi husika na inazuia maendeleo na ustawi wa Dunia.

Msemaji huyo amesema China inaamini katika mshikamano, ushirikiano na uwazi badala ya migawanyiko, mapambano na kujitenga.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha