Watu zaidi milioni 300 wasafiri kwa njia ya reli wakati wa pilika za safari nyingi za Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2024

Abiria wakisubiri kupanda treni zao katika Stesheni ya Reli ya Zhengzhou Mashariki huko Zhengzhou, Mkoa wa Henan, Katikati ya China, Januari 26, 2024. (Xinhua/Li An)

Abiria wakisubiri kupanda treni zao katika Stesheni ya Reli ya Zhengzhou Mashariki huko Zhengzhou, Mkoa wa Henan, Katikati ya China, Januari 26, 2024. (Xinhua/Li An)

BEIJING - Watu zaidi milioni 300 wamesafiri kwa njia ya reli kutoka Januari 26 hadi Februari 19, siku 25 za kwanza za pilika za safari nyingi kwa ajili ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, kwa mujibu wa Shirika la Kampuni za Reli za China.

Sekta ya reli ya China imesema abiria milioni 14.04 wamesafiri katika siku ya Jumatatu, huku idadi hiyo katika Jumanne ikikadiria kufikia milioni 13.3.

Shirika hilo la reli limeendelea kuwa na shughuli nyingi hata baada ya kumalizika kwa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, huku wanafunzi na wafanyakazi vibarua wakiendelea kusafiri kwa reli.

Idara za reli zimetoa treni za ziada ili kukabiliana na mahitaji ya usafiri. Pia zimetekeleza hatua za maandalizi za kukabiliana na theluji na barafu katika sehemu mbalimbali za China ili kuhakikisha usafiri baada ya likizo.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ambayo iliangukia Februari 10 mwaka huu, ni sikukuu kubwa zaidi ya jadi ya China. Pilika za safari nyingi kwa ajili ya sikukuu hiyo mwaka huu zilianza Januari 26 na zitakamilika Machi 5.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha