Mjumbe wa China atoa wito wa kuendelea kuiunga mkono Somalia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2024

UMOJA WA MATAIFA - Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw.Zhang Jun siku ya Jumatatu ametoa wito wa kuunga mkono juhudi za Somalia za kufikia utulivu wa kisiasa, mpito wa usalama, na ujenzi mpya wa kiuchumi na kijamii.

Kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Somalia, Bw. Zhang amesema kwamba ufuatiliaji makini na uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kwa Somalia lazima usitetereke, kwani Mwaka 2024 ni muhimu kwa mchakato wa kisiasa, mpito wa usalama na ujenzi mpya wa nchi hiyo.

Amesema China inaunga mkono pande zote nchini Somalia katika kutatua tofauti zao kwa njia ya mazungumzo na mashauriano na kuhimiza zaidi mpito wa kisiasa.

"Ikumbukwe kwamba kuchagua mfumo wa kisiasa na njia ya maendeleo ni suala la ndani la Somalia. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kutilia maani kanuni inayoongozwa na inayomilikiwa na Wasomali na kuepuka kulazimishwa kwa nguvu kwa mtindo wa utawala uliowekwa kwa nguvu kutoka nje," amesema.

Kwa upande wa mpito wa usalama wa Somalia, Zhang amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunga mkono Serikali ya Muungano ya Somalia katika kuimarisha mafanikio ya mapambano dhidi ya ugaidi na kudumisha utulivu katika kipindi kilichopita.

Ni muhimu kusaidia idara za usalama za Somalia katika kujenga uwezo wao wa kubeba jukumu kubwa la usalama, ameongeza.

Pia kuna haja ya kusaidia ujenzi mpya wa kiuchumi na kijamii wa Somalia, Zhang amesema.

Amesema, China inakaribisha kutolewa hivi karibuni kwa “Matarajio ya Miaka Mia Moja 2060” na serikali ya Muungano ya Somalia kwa ajili ya kuweka kazi muhimu kwa maendeleo ya nchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha