Waziri wa Mambo ya Nje wa China asisitiza hali ya kunufaishana ni mustakabali wa binadamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), anafanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Hispania Jose Manuel Albares mjini Cordoba, Hispania, Februari 18, 2024. (Picha na Gustavo Valiente/Xinhua)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), anafanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Hispania Jose Manuel Albares mjini Cordoba, Hispania, Februari 18, 2024. (Picha na Gustavo Valiente/Xinhua)

CORDOBA, Hispania - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesisitiza umuhimu wa njia za kunufaishana kwa mustakabali wa binadamu siku ya Jumapili kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Hispania Jose Manuel Albares katika mji wa Cordoba, Kusini mwa Hispania.

Kutonufaishana siyo chaguo la busara, na njia za kunufaishana zinapaswa kuwa mustakabali wa binadamu, amesema Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.

Kauli hiyo ya Wang ilitokana na maswali kuhusu "mienendo ya kutonufaishana" iliyoangaziwa katika Ripoti ya Usalama ya Munich 2024. Amebainisha mambo matatu yanayochangia katika hali hii ya hatari ni kwamba: kucheza michezo ya kunufaisha upande mmoja, kutengana kiuchumi na kukata minyororo ya usambazaji, na kuchochea mapambano kati ya makundi tofauti.

Vitendo hivi vinaumiza maslahi ya wengine bila kujinufaisha, vinashusha maendeleo na ustawi wa Dunia, vinavuruga sana juhudi za kukabiliana na changamoto za kimataifa, na kumomonyoa kwa kiasi kikubwa msingi wa amani na maendeleo duniani, amesema.

Matokeo ya kutonufaishana lazima yaepukwe na pande zote, Wang amesema, akibainisha kuwa nchi nyingi zaidi sasa zinafahamu hili.

Ametoa wito wa kutafuta kwa pamoja hali ya kunufaishana, akizitaka nchi kuungana badala ya kugawanyika, kuzingatia maslahi ya msingi ya kila upande, kutupilia mbali upendeleo wa kiitikadi, na kukataa mapambano kati ya makundi tofauti.

Huku akitetea ushirikiano badala ya mapambano, kufanya mazungumzo badala ya migogoro, kufanya mashauriano badala ya jeuri na usawa badala ya ubabe, Wang pia amezugumzia kushikilia kufungua mlango, kulinda utulivu wa minyororo ya uzalishaji na usambazaji, na kuboresha mfumo wa biashara huria unaoongozwa na WTO.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha