Waziri Mkuu wa DRC ajiuzulu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2024

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)Sama Lukonde Kyenge (kushoto) akiwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Felix Tshisekedi huko Kinshasa, Mji Mkuu wa DRC, Tarehe 20, Februari. (Picha kutoka Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo/kupitia Xinhua)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Sama Lukonde Kyenge (kushoto) akiwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Felix Tshisekedi huko Kinshasa, Mji Mkuu wa DRC, Tarehe 20, Februari. (Picha kutoka Ikulu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo/kupitia Xinhua)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) Sama Lukonde Kyenge amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Felix Tshisekedi, ofisi ya rais ya DRC imetangaza siku ya Jumanne kwenye mtandao wa X, ambao zamani uliitwa Twitter.

Sama Lukonde Kyenge aliteuliwa kuwa waziri mkuu Februari 15, 2021.

Tarehe 8, Februari, Mahakama ya Katiba ya DRC ilitangaza uamuzi wa kutoshabihiana kwa majukumu ya mamlaka ya serikali na mamlaka ya kutunga sheria, ikiwataka mawaziri, magavana wa majimbo na wahudumu wa baraza la serikali, ambao pia wamechaguliwa katika uchaguzi wa bunge, kujiuzulu kutoka kazi zao za kisiasa, isipokuwa kama watakana mamlaka za kuchaguliwa kwao katika chaguzi.

Desemba 20, 2023, viongozi wa serikali 31 kati ya 60, akiwemo waziri mkuu, walichaguliwa kuwa wabunge katika uchaguzi mkuu, ambao karibu wapiga kura milioni 44 walikwenda kwenye vituo vya kupiga kura siku hiyo ili kuchagua rais mpya, wabunge wapya, pamoja na wajumbe wa majimbo na manispaa.

Tarehe 7, Februari, Felix Tshisekedi alimtangaza Augustin Kabuya Tshilumba, katibu mkuu wa chama tawala cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS) kuunda serikali mpya. Chama hicho kilishinda viti 69 katika viti 500 vya Bunge la Taifa kikiongoza vyama vingine 44 katika chaguzi kuu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha