Makamu wa Rais wa Tanzania asema lugha mama zina mchango mkubwa katika kukuza uchumi

(CRI Online) Februari 21, 2024

Makamu wa Rais wa Tanzania Philip Mpango ametoa wito wa kukuza lugha mama, akisema zina jukumu muhimu katika kuhimiza ukuaji wa uchumi.

Akiongea katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Nafasi za Lugha Mama lililofanyika jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania, Mpango amesema kuwa matumizi ya lugha mama yanaweza kupanua ushiriki wa watu wengi katika fursa za kiuchumi na kibiashara.

Ameongeza kuwa watu wengi wanaotegemea lugha zao mama wanaweza kushiriki katika fursa za kiuchumi na biashara kama lugha zao zitashughulikiwa.

Maadhimisho hayo ya kila mwaka ya Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama yanayofanyika Februari 21 yanalenga kukuza uelewa wa lugha na tamaduni anuwai na kukuza lugha nyingi.

Mpango pia ameutaka mkutano huo kujadili jinsi lugha mama zinavyoweza kuwa na nafasi katika uchumi wa kidijitali.

Mkutano huo wa siku mbili umewaleta pamoja viongozi waandamizi wastaafu, wanadiplomasia, watunga sera, wafanyabiashara wenye viwanda, wasomi, viongozi wa dini, vijana, wanawake na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka sehemu mbalimbali duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha