Lugha Nyingine
UNOCHA laomba dola bilioni 2.6 ili kukabiliana na mzozo wa kutisha nchini DRC
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na washirika wake wa kibinadamu wametoa ombi la dola bilioni 2.6 za Kimarekani ili kufadhili mpango wa kutoa misaada ya kibinadamu wa mwaka 2024 nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa Jumanne na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (UNOCHA), fedha hizo zinalenga kutoa msaada wa kuokoa maisha na ulinzi kwa watu milioni 8.7 wenye uhitaji.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja, mzozo wa kibinadamu nchini DRC umefikia viwango vya kutisha, huku ongezeko jipya la ghasia, hasa mashariki mwa nchi hiyo, likilazimisha waathirika kuhama makazi yao.
Mratibu Mkazi na Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Bruno Lemarquis amesema mgogoro wa kibinadamu nchini DRC umefikia hatua mpya mwaka huu kutokana na kuongezeka kwa mizozo, kuibuka kwa mivutano mipya, na majanga yanayohusiana na hali ya hewa.
Amesema, kutokana na hali hii, kuna wanaume, wanawake na watoto wanaokabiliwa na mazingira magumu sana.
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
Ndege C919 ya China yashiriki mazoezi ya Maonyesho ya Anga ya Singapore
Chuo Kikuu cha Kenyatta chafanya maonyesho ya dragoni wa China ili kukuza mawasiliano ya kitamaduni
Mkoa wa Xizang, China wafungua maeneo ya utalii kwa umma bila tiketi ili kuhimiza utalii
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma