

Lugha Nyingine
Dar es Salaam yapata mkopo wa Benki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha miundombinu
(CRI Online) Februari 21, 2024
Benki ya Dunia Jumanne iliidhinisha mkopo wa Euro milioni 361.1 (sawa na dola takriban milioni 390 za kimarekani) kwa ajili ya utekelezaji wa kipindi cha pili cha Mradi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP).
Taarifa iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema kipindi cha pili cha mradi huo kitahusisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita zaidi ya 200 na miundombinu ya mifereji yenye urefu wa kilomita 300, ikiwa ni pamoja na kufanyia marekebisho maduka, vituo vya mabasi, bustani na vituo muhimu vya jiji.
Waziri wa Fedha wa Tanzania Mwigulu Nchemba na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia anayeshughulikia mambo ya nchi za Malawi, Tanzania, Zambia and Zimbabwe Nathan Belete wamesaini makubaliano ya mkopo huo jijini Dar es Salaam.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma