China yaanzisha mfumo wa uratibu wa kukusanya mitaji kwa miradi ya nyumba katika miji 214

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 22, 2024

Picha hii iliyopigwa Juni 7, 2023 ikionyesha mandhari ya Mji wa Changsha, Mkoa wa Hunan, Katikati ya China. (Xinhua/Chen Sihan)

Picha hii iliyopigwa Juni 7, 2023 ikionyesha mandhari ya Mji wa Changsha, Mkoa wa Hunan, Katikati ya China. (Xinhua/Chen Sihan)

BEIJING - Miji jumla ya 214 katika mikoa 29 nchini China ilikuwa imeanzisha mfumo wa uratibu wa kukusanya mitaji kwa miradi ya nyumba hadi kufikia Februari 20, ikiwa ni sehemu ya juhudi za China za kuhimiza maendeleo mazuri ya soko la nyumba.

Wizara ya Nyumba na Ujenzi wa Miji na Vijiji ya China ilisema Jumanne kwamba imetoa makundi ya "orodha nyeupe" inayohusisha miradi 5,349 ya nyumba inayostahiki msaada wa kifedha na kuituma kwa benki za biashara.

Wizara hiyo imesema, hadi sasa, miradi ipatayo 162 katika miji 57 imepokea ufadhili wa benki wenye thamani ya yuan jumla ya bilioni 29.43 (kama dola bilioni 4.14 za Marekani).

Takwimu zilizotolewa na Benki ya China, Benki ya Ujenzi ya China, Benki ya Kilimo ya China, Benki ya Akiba ya Posta ya China na baadhi ya benki za hisa zimeonesha kuwa, Serikali za mitaa na taasisi za fedha zimekuwa zikifanya juhudi za kufuata mfumo huo wa uratibu, huku mikopo yenye thamani ya yuan bilioni 123.6 ikiidhinishwa kwa miradi ya nyumba iliyoorodheshwa.

Mwezi Januari China ilitangaza mpango wa kuanzisha mfumo wa uratibu wa kukusanya mitaji kwa miradi ya nyumba kwa lengo la kukidhi mahitaji ya ukusanyaji halali wa mitaji kwa miradi ya nyumba na kusaidia ukuaji mzuri ulio tulivu wa soko la nyumba la China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha