Roboti zafanya kazi ya kilimo katika kitongoji cha Shanghai

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 22, 2024

Mhandisi akiendesha roboti ya kilimo katika eneo la Shamba la Diantian huko Shanghai, China, Januari 25. (Picha na Zhao Yihe/Xinhua)

Mhandisi akiendesha roboti ya kilimo katika eneo la Shamba la Diantian huko Shanghai, China, Januari 25. (Picha na Zhao Yihe/Xinhua)

Kazi za kilimo za vijijini kwa muda mrefu zimekuwa zikihusishwa kwa karibu na ng’ombe, plau na kazi ya kuchosha. Siku hizi, pia kuna roboti za kilimo na mashine nyingine za aina mbalimbali zenye akili mnemba, ikiashiria mageuzi muhimu katika kazi za kilimo.

Kwenye Shamba la Diantian katika kijiji kilichoko Shanghai, mageuzi hayo yanaonekana dhahiri. Hapa roboti zinazoendeshwa na wahandisi zimekuwa mbadala wa kilimo cha jadi cha kutumia ng’ombe.

Kwa jumla wapo wahandisi zaidi ya 70 wanaofanya kazi katika Ushirika wa kijiji wa Diantian, ambako mpunga ni zao kuu.

Katika miaka saba iliyopita, wahandisi hao wamekuwa wakishiriki kwenye utafiti na uendelezaji wa kilimo, na kuwezesha kuundwa kwa aina zaidi ya 60 za roboti za kilimo zinazoweza kufanya kazi kuanzia zile za kupanda hadi kuvuna.

Roboti hizo hutumia magurudumu ya kutambaa kwenye ardhi ambayo yanaweza kuendana na kufanya kazi katika aina mbalimbali za ardhi, huku mfumo wao wa uendeshaji wenye akili mnemba ukihudumu kama ubongo wa kupanga mwendo wao.

Wakulima wanahitaji tu kutumia simu zao kuwasha roboti hizo. “Nilikulia kijijini, na ninajua kazi za kilimo zinaweza kuwa za kuchosha sana,” amesema Wang Jinyue, kiongozi wa Ushirika wa Kilimo wa Diantian.

Tofauti na siku za nyuma, mstari mrefu wa roboti za kilimo zipo zinazunguka shambani kusaidia kazi za kilimo leo.

Zinafanya kazi kwa ufanisi, usahihi na bila ya kuchoka, amesema Wang, akisisitiza kuwa teknolojia kama vile 5G, utambuzi wa picha na data kubwa zinawezesha roboti hizo kupima kwa kasi umbali wa kati ya mazao na kukamilisha uvunaji wa kasi ndani ya sekunde kadhaa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Kilimo na Vijiji ya China, kiwango cha mchango wa sayansi na teknolojia ya kilimo nchini China kimezidi asilimia 62 mwaka 2022.

Picha hii iliyopigwa Januari 25, 2024 ikimwonesha Wang Jinyue (kwanza kushoto), ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Teknolojia ya AI ya Shanghai Sweet, ikikagua roboti ya kilimo pamoja na wahandisi katika Shamba la Diantian la kitongoji cha Tinglin cha Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Zhao Yihe)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha